Uasin Gishu: Baa ya Kesogon eneo la Ziwa Yafugwa

/

Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu imetangaza kufungwa kwa baa ya Kesogon katika soko la Ziwa eneo bunge la Soy.

Maafisa wa Idara ya Afya katika kaunti hiyo waliongoza shughuli ya kufungwa kwa baa hiyo Ijumaa.

Kulingana na Afisa Mkuu wa Afya anayesimamia kitengo cha kuzuia maambukizi Joyce Sang, baa hiyo imefungwa kutokana na wasiwasi wa mchango wake katika kuenea kwa ugonjwa wa kifua kikuu.

Bi Sang akiangalia baadhi ya vileo vilivyokuwa vikiuzwa katika baa hiyo ya Kesogon.
Bi Sang akiangalia baadhi ya vileo vilivyokuwa vikiuzwa katika baa hiyo ya Kesogon.

Kifua Kikuu ni ugonjwa ambao unaathiri zaidi mapafu, na unaweza kusambazwa kwa urahisi katika maeneo yenye watu wengi au yenye hewa duni kama vile baa.

Uamuzi wa kufunga Kesogon Baa ni hatua madhubuti tunayochukua kama Idara ya Huduma za Afya ili kupunguza hatari ya maambukizo ya kifua kikuu ndani ya jamii,” Sang amesema.

Kwa kufunga eneo hili la biashara, tunalinda umma dhidi ya uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa huo na pia kuzuia kuenea kwake zaidi,” aliongeza.

Athari za pombe

Sang aidha amebainisha kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi umehusishwa na matatizo mengi ya kiafya, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa ini, matatizo ya moyo, mishipa, na matatizo ya afya ya akili.

Kwa kufuatilia kwa karibu uzalishaji, usambazaji na unywaji wa vileo, tunaweza kukuza tabia ya unywaji wa kuwajibika na kupunguza hatari zinazohusiana na afya kwa sababu unywaji pombe kupita kiasi unaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya uhalifu, vurugu na usumbufu wa kijamii,” anasema Afisa huyo wa Afya.

Maafisa wa Afya wakiwa na wenyeji wa eneo la Ziwa.
Maafisa wa Afya wakiwa na wenyeji wa eneo la Ziwa.

Idara ya Huduma za Afya ina jukumu muhimu katika kuhakikisha ustawi wa umma kwa kudhibiti uzalishaji, usambazaji na unywaji wa vileo hivyo kulinda afya na usalama wa wakazi.

Mbali na kufungwa kwa eneo hilo la kuuzia vileo, Sang pia amezindua uhamasishaji wa ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Hii ni baada ya baadhi ya watu waliokuwa wakishukiwa kuwa na ugonjwa huo kufariki.

Wakati wa hafla hiyo, Sang ametoa wito kwa wananchi kuenda kwa upimaji wa bure.

Zoezi hilo litadumu kwa muda wa wiki moja.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Previous Story

Counties Have Increased Own-source Revenue Collection – CRA

Next Story

Arnesens Boys, Moi Girls Start Title Defence With Huge Wins

Latest from County