Baraza la kitaifa la ushauri katika dini ya Kiislamu (Kenya National Fatwa Council) limeelezea kusikitishwa na hatua ya waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki kutangaza Jumatano kama sikukuu ya kusherehekeha Eid al-Adha.
Mwenyekiti wa baraza hilo Shariff Ahmad Ahmad Badawi anasema Waziri Kindiki alitoa uamuzi huo hata baada ya wao kumuandikia barua wakimshauri tarehe mwafala ya sherehe hizo.
Kwenye mahojiano na Uasin Gishu News kwa njia ya simu, Badawi amesema kama Baraza, walipendekeza Alhmisi kuwa sikukuu ya kuwaruhusu waislamu kusherehekea Eid al-Adha kutokana na mwandamo wa mwezi katika eneo la Africa mashariki, hasa Kenya, Tanzania na Zanzibar.

“Tunasikitishwa na uamuzi wa waziir Kindiki kupeana sikukuu Jumatano badala ya Alhamisi kama sisi tuliyopendekeza,” Badawi alisema.
“La kusikitisha zaidi ni kuwa hata baada ya sisi kumuandikia barua, waziri hakutujibu, na badala yake akatoa gazeti rasmi la serikali akiwema Jumatano ndio siku ya kusherehekea Eid al-Adha,” aliongeza.
Kauli sawa na hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Baraza hilo Sheikh Abubabar Bini.
Muingilio wa kisiasa
Kulingana na Bini, kwa miaka michache iliyopita, uamuzi kuhusu siku ya kusherehekea Eid hutolewa baada ya siku 30 za mfungo, lakini hilo limebadilika hii maajuzi.
Ameelezea hofu kuwa huenda utoaji wa gazeti rasmi la serikali kuhusu sherehe za Waislamu umeingiwa kisiasa.

Sasa amependekeza mabadilio ya sheria ili kuhakikisha kuwa hakuna muingilio wa kisiasa kwenye mchakato wa kubaini sikukuu ya sherehe mbalimbali za waislamu nchini Kenya.
“Tunataka mabadiliko ya sheria ili kwamba inabainika wazi siku flani ni ya sherehe Fulani – kama ilivyo na sherehe za Pasaka kwa ndugu zetu wa Kikristo. Sheria haifai kutoa nafasi ya swala kama hili kuingiliwa kiasiaa,” Sheikh Bini alisema.
Waziri Kindiki alitangaza Jumatano sikukuu kwa sherehe za Eid al-Adha
Sherehe hizi zinatoa nafasi kwa Waislamu kufanya maombi na kuchinja, kama njia mojawapo ya kuadhimisha Mtume Ibrahimu ambaye alijitolea kumtoa mwanawe Ishmaeli wakati Mungu alimhitaji afanye hivyo.


