Viongozi wa Kiislamu Kazkazini mwa bonde la Ufa wametoa wito kwa Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kufanya mazungumza ili kutatua utata uliopo nchini.
Kulingana na mweyekenye wa Baraza la Maimamu na Wahubri wa Kiislamu (CIPK) eneo hilo Abubakar Bini, wakati huu ambapo Waislamu wameingia katika mwaka mpya, ipo haja ya utulivu kuwepo nhini.
Bini akizungumza mjini Eldoret amesema kwa mujibu ya dini ya Kiislamu, kila mara wanaposherehekea kuanza kwa mwaka mpya na miezi mingine mitukufu, iwapo kuna vita husitishwa.
“Kwa kuwa tulioko mwezi huu ni mwezi mtukufu, tungeomba tuwe na utulivu. Kuwe na mazungumzo na uwiano sababu ya kuheshimu mwezi mpya wa Kalenda ya kiislamu,” alisema kiongozi huy wa CIPK.

Muungano wa Upinzani – Azimio umekua ukifanya maandano tangu Jumatano ukishinikiza kushuka kwa bei ya bidhaa na kutupiliwa mbali kwa sheria mpya ya kifedha.
Maandano hayo yamekuwa yakishuhudiwa katika maeneo mbali mbali nchini ikiwemo jiji kuu la Nairobi.
Waisilamu kote ulimwenguni walisherehekea kuanza kwa mwaka mpya wa 1445 hapo Jumatano.
Hii ni kwa mujibu wa Kalenda ya Kiislamu ambayo inaambatana na kughura kwa Mtume Muhammed kutoka Madina kuelekea Mekka.
“Waislamu wana kalenada yao – Kalenda Hijiria iliweke siku ya Mtume Mohammed kutoka Madina kuenda Mecca ndio ikawekwa mwezi huu wa mfungo nne,” alielezea Bini ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa baraza la ushairi wa maswala ya Kiislamu Nchini Kenya – Fatwa.
“Waislamu kila kitu wanafanya kulingana na kalenda. Kwa mfano Hajji ni mwezi wa kumi na moja na kumi na mbili – Hajji ni mwezi maalum, huwezi fanya Haji kwa miezi mingine na huwezi pata hilo pasi kufuata kalenda,” aliongeza.


